- Get link
- X
- Other Apps
Ngozi ni makighafi asilia itokanayo na wanyama kama vile ng'ombe, mbuzi, kondoo, nyumbu, n.k. Ngozi hutumika kutengeneza bidhaa mbali mbali kama vile mabegi, viatu, mikoba, waleti/pochi, mikanda, n.k.
Kuna aina tofauti za ngozi; ambapo kuna ngozi za kiwandani na ngozi za wanyama. Ngozi za kiwandani hutumia malighafi ambazo si asilia na kemikali na Kisha kupewa muonekano wa ngozi asilia. Ngozi ya kiwandani imegunduliwa kama mbadala wa ngozi asilia ili kupata bidhaa zenye muonekano wa ngozi kwa bei rahisi.
Ngozi za wanyama pia zipo katika matabaka tofauti ambapo ngozi ya tabaka la juu zaidi ndio yenye bei kubwa na hufahamika kwa jina la "top-grain leather".
Wapenzi wengi wa mabegi, viatu na mikanda ya ngozi wamekua wakikimbilia kwenye bidhaa za mtumba za ngozi ili kuweza kupata vitu vya ngozi kwa bei rahisi ambapo bidhaa nyingi mpya za ngozi zinakua ni bei juu.
Unapokua unatembelea kurasa mbali mbali za wauzaji na wasambazaji wa bidhaa za ngozi mtandaoni au unapokwenda kwenye maduka ya bidhaa za ngozi, unaweza ukajiuliza, je hizi bei ninazoziona tumewekewa sisi sisi Watanzania au ni kwa ajili ya watalii na watu spesho ama kuna kundi maalumu la watu wanaotakiwa kununua bidhaa hizi.
Mfano begi jipya la ngozi linaanzia 100,000Tshs mpaka 400,000Tshs na kuendelea wakati kwa mabegi ya matirio nyengine utanunua kwa Tshs 50,000 mpaka 80,000Tshs kwa begi jipya.
Wakati viatu vipya vya ngozi asilia huanzia Tshs 100,000 na kuendelea juu kulingana na tabaka la ngozi lilitumika kutengeneza kiatu hicho.
Swali linakuja," Je! Ni kwa nini bidha za ngozi zinauzwa kwa bei ya juu zaidi ya bidhaa zengine?"
LeatherbagsTz tunakuletea sababu kuu tatu zinazofanya bei za bidhaa za ngozi kuwa juu. Ambazo ni kama zifuatazo:-
- Maandalizi ya ngozi.
- Ishara ya ufahari.
- Kudumu na kuvutia
1. Maandalizi ya ngozi.
Ngozi ni bidhaa ambayo inategemeana zaidi na mahitaji ya nyama. Pale ambapo mahitaji ya nyama yanapokua juu, ngozi hupatikana kwa urahisi kuliko pale ulaji na uhitaji wa nyama unapokuwa chini kwani mabucha na wasindikaji wa nyama huchinja wanyama wachache na hivyo ngozi kuwa chache.
Pia ngozi ya kutengeza bidhaa kama mabegi, viautu, nk hupatikana kwa wanyama ambao wamekomaa wenye umri kuanzia mwaka mmoja na kuendelea hivyo huchukua muda mrefu kuweza kupata ngozi inayofaa.
Vile vile, kabla ya ngozi kutumika kiwandani, inahitaji kupitia hatua mbali mbali za kuweza kukfanya isioze, isinuke na kuipa muonekano mzuri zaidi kwa kubadili rangi au kuipa "pattern" nzuri. Kazi hii hufanywa na wataalamu ambao ni wanalipwa Mishawaka mikubwa.
Pia bidhaa nyingi za ngozi hushonwa kwa mikono ambapo inachukua muda mrefu na kuhitaji umakini zaidi kwani pale unapokosea kushona au kukata ngozi usababisha alama(scar) ambayo hushusha thamani ya bidhaa za ngozi. Hivyo maandalizi ya bidhaa za ngozi ambapo hutumika muda mwingi, umakini zaidi, wataalamu na upakinaji wa ngozi hufanya bei za bidhaa za ngozi kuwa juu zaidi.
2. Ishara ya ufahari:
Enzi za zamani ngozi na bidhaa za ngozi vilitumika kama mfumo wa malipo mpaka pale madini ya fedha, zahabu na chuma yalipogundulika na kuundwa kwa pesa za sarafu na kuanza kutumika katika malipo.
Leo hii kuna ka hali flani ka ufahari pale unapobeba begi la ngozi asilia au pale unapovaa kiatu cha ngozi orijino. Mabegi ya ngozi hutumika kubeba vitu vya thamani kama vile laptop, simu, nyaraka nk.
Wengi wanaamini unapovaa kiatu cha ngozi, mkanda wa ngozi au kubeba begi/pochi ya ngozi asilia, unakuwa katika drama moja la juu zaidi na la kipekee tofauti na wengine, hivyo basi na bei inakuwa ni tofauti ukilinganisha na bidhaa zengine ambazo sio za ngozi.
3. Kudumu na kuvutia:
Bidhaa za ngozi asilia zina uwezo wa kudumu kwa muda mrefu kuanzia miaka mitano mpaka kumi na kuendelea juu. Kikubwa ni kuzingatia utunzaji wa bidhaa hiyo kama kuepuka kuwa mbichi au kuiweka juani kwa muda mrefu.
Wengi wanapotelea dukani kwetu kununua begi ama bidhaa nyengine za ngozi huja na kauli moja amba ni, " Nahitaji mkataba" akimaanisha anahitaji bidhaa ambayo atadumu nayo kwa muda mrefu zaidi.
Pia bidhaa za ngozi zinakuja na dizaini (muonekano) za kipekee na kuvutia.
Mfano, ukienda kwenye kikao na kuona "messenger laptop bags or vintage bags" kwenye meza za mabosi, nafsi yenyewe inasema, ndio, nahitaji kabegi kama haka na mimi.
Hivyo bidha za ngozi zinakua ni za gharama kutokana na upatikanaji wa ngozi na pia unalipia gharama zaidi kwa zile sifa kuu za ngozi za kudumu, kuvutia na kukufanya kuwa daraja moja juu zaidi ya wengine, " the luxury class".
Kwa mahitaji ya bidha za ngozi tupigie simu namba 0687751572 au tembelea page yetu ya instagram, @leatherbags_and_shoes.
Asante kwa kufatilia nakala hii.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment